Header Ads Widget

TCU YAONGEZA MUDA WA UDAHILI KWA SHAHADA YA KWANZA KWA PROGRAMU AMBAZO BADO ZINA NAFASI


Na Lilian Kasenene,Morogoro 

TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imeongeza awamu ya tatu ya udahili baada ya kupokea maombi kutoka kwa wadau vikiwemo vyuo vikuu na jumuiya ya wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya juu Tanzania (TAHLISO).

Kuongezwa kwa awamu hiyo ya tatu ambayo itaanza Oktoba 6 hadi oktoba 10,2025, ni baada ya awamu mbili zote za udahili kukamilika.

Katibu mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU Profesa Charles Kihampa alitoa taarifa hiyo alipozungumza na Waandishi wa Habari mkoani Morogoro.

Prof Kihampa alisema TCU baada ya kupokea maombi ya kuongeza muda wa kutuma maombi ya udahili kutoka kwa wadau wao kwa ajili ya waombaji ambao hawakufanikiwa kupata udahili katika awamu zilizopita na kwa programu ambazo bado zina nafasi.

"Tume imeongeza muda wa udahili kwa kufungua Awamu ya Tatu na ya mwisho ya udahili na itakayoanza tarehe 06 hadi 10 Oktoba, 2025,"alisema.

Mtendaji huyo alitoa ushauri kwa waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi ya udahili au hawakuweza kupata nafasi ya kudailiwa katika awamu zilizopita kutokana na sababu mbalimbali watumie fursa hiyo kwa kutuma maombi yao ya udahili kwenye vyuo wanavyovipenda.

Aidha alisema Tume inaelekeza vyuo vya Elimu ya juu nchini kuendelea kutangaza programu ambazo bado zina nafasi na waombaji udahili na vyuo wanapaswa kuzingatia utaratibu wa udahili wa awamu ya tatu.

Alitoa wito kwa waombaji waliodahiliwa katika Chuo zaidi ya kimoja katika Awamu ya Pili na wale ambao hawakuweza kuthibitisha udahili katika Awamu ya Kwanza, wanapaswa kuthibitisha udahili wao katika chuo kimojawapo kuanzia tarehe 06 hadi 19 Oktoba, 2025. 

"Uthibitisho huo unafanyika kwa kutumia namba maalum ya şırı iliyotumwa kwa ujumbe mfupi kupitia namba zao za simu au barua pepe walizotumia wakati wa kuomba udahili,"alisema.

Alisema wale ambao hawatapata kwa wakati ujumbe huo, wanashauriwa kuingia kwenye mifumo ya udahili ya vyuo walivyodahiliwa na kuomba kutumiwa namba hiyo ili kuweza kujithibitisha katika chuo husika.

Aidha, alisema uthibitisho wa udahili ufanyike kupitia akaunti ambayo muombaji alitumiawakati wa kuomba udahili. Kwa urahisi wa rejea, orodha ya majina ya waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja itapatikana kwenye tovuti ya TCU(www.tcu.go.tz) 06 Oktoba, 2025.

Udahili katika awamu zote mbili kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza katika Taasisi za Elimu ya Juu nchini kwa mwaka wa masomo 2025/2026 umekamilika.Majina ya waliodahiliwa katıka Awamu ya Pili yatatangazwa na vyuo husika kuanzia 06 Oktoba, 2025.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI