Header Ads Widget

MTOTO WA ROBERT MUGABE AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA DAWA ZA KULEVYA

 

Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amefikishwa katika mahakama ya Harare akikabiliwa na shtaka la kupatikana na dawa za kulevya.

Robert Mugabe Jr, 33, alikamatwa Jumatano asubuhi alipokuwa akiendesha gari kwa njia isiyo sahihi katika barabara ya njia moja, kulingana na hati za mahakama.

Polisi walipekua begi jeusi alilokuwa amevaa wakati huo na inadaiwa walipata sacheti mbili ndogo za bangi.

Kufuatia tukio hilo, polisi walisema katika taarifa kwamba watu watano "waliohusishwa naye" pia walikamatwa.

Wakili wa Bw Mugabe alisema wanapanga kukana mashtaka, na kupinga madai yaliyotolewa na polisi.

Bw Mugabe aliyekuwa amevaa kofia nyekundu huku akiwa anazungumza na simu yake alipokuwa akiongozwa kwenda katika mahakama ya hakimu siku ya Alhamisi. Alizungukwa na watu na hakuwa amefungwa pingu.

Mahakama ilimweka rumande Bw Mugabe akisubiri uamuzi wa dhamana siku ya Ijumaa.

Polisi wamesema wataendelea na uchunguzi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI