Header Ads Widget

TANESCO SACCOS YATOA MIKOPO YA SH 27 BIL KWA WANACHAMA WAKE

 

Na Lilian Kasenene,Morogoro

Matukio Daima Media 

CHAMA cha Ushirika wa Akiba na mikopo cha Shirika la umeme Tanzania(TANESCO SACCOS) kimefanikiwa kutoa mikopo ya zaidi ya sh 27.2 bilioni kwa wanachama wake kwa kipindi cha Mwaka mmoja.

Akitoa taarifa kwa wanachama wakati wa  Mkutano mkuu wa 57 wa TANESCO SACCOS mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO SACCOS Omari Shaaban alisema wametoa mikopo kwa wanachama 4,031 ambayo ni kuanzia Januari hadi Agosti 2025 ikiwa ni sehemu ya mafanikio ya uwanzishwaji wake katika kuwasaidia kiuchumi.

"Fedha hizi 27,257,207,164 ni Mikopo ilitolewa kwa kufuata taratibu na vigezo vilivyowekwa na chama kupitia sera ya mikopo, ikiwemo kufanya tathmini ya uwezo wa mkopaji, kuhakikisha kuwepo kwa wadhamini wa kuaminika, na kuzingatia uwezo wa marejesho ya kila mwanachama,"alisema Shaaban.

Akizungumzia suala la mtaji mwenyekiti huyo alisema Mtaji wa chama umeongezeka kutoka sh 4,090,957,554 mwaka 2023 hadi kufikia sh 7,149,494,412 mwaka 2024 sawa na ongezeko la asilimia 75.

Kuhusu hisa za wanachama kwa mwaka ulioishia 31 Disemba, 2024 ziliongezeka kwa asilimia 5 na kufikia kiasi cha sh 11,184,586,538 ukilinganisha na mwaka 2023 ambapo zilikuwa na thamani ya sh 10,626,604,028.

Mwenyekiti Shaaban alieleza juu akiba za wanachama ambazo zimeongezeka kutoka sh 44.74,  2023, hadi kufikia sh 46.9, 2024 na kufanya ongezeko la asilimia 5  na kwamba Chama kimetoa faida juu ya akiba kiasi cha sh 907,161,712.

Akimwakilisha mkurugenzi mtendaji wa TANESCO wakati wa ufunguzi mkutano mkuu huo wa 57, naibu mkurugenzi mtendaji uzalishaji wa Tanesco Antony Mbushi alisema Tanesco inajivunia  uwepo wa saccos hiyo ikiwemo maamuzi ya kuongeza kwa kufuata taratibu na vigezo vilizowekwa na wananchama kupitia sera zinazofuata Sheria zote za mikopo.

Aidha Mbushi akautaka uongozi kuendelea kutoa misaada kwenye maeneo mengine ili kuhakikisha wanafikia lengo na kutoishiankutoa mashukanya hospitali tu bali iwe pia kwa watu wenye mahitaji wengine.

Naye Wilson Kingu mjumbe wa mkutano huo kutoka Kahama Shinyanga alisema saccos yao imekuwa ya thamani na mkombozi kwao kiuchumi kwani anauwezo wa kukopa fedha kubwa na kurejesha.

Neema Francis mwakilishi mkutano huo kutoka Morogoro akatoa wito kwa Wafanyakazi wenzake kujiunga kwenye chama kwani kinasaidia katika maisha binafsi na kupiga hatua kwa haraka kupitia Bodi yake .

Tanesco saccos kupitia bodi yake inatarajia kutekeleza mpango wa Chama kumiliki jengo la ofisi katika kiwanja chetu kilichopo Kijitonyama, Dar es Salaamam ambapo hatua hiyo itawezekana baada ya wanachama wote kukubali pendekezo la kununua hisa za jengo kuanzia mwaka wa fedha Januari 2026.

Mpango wa kugharamia ujenzi utahusisha kuanzishwa kwa akaunti ya hisa za jengo na akiba ya jengo.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI