Header Ads Widget

MUTHARIKA WA MALAWI AAPISHWA KWA MUHULA WA PILI KUWA RAIS

Peter Mutharika wa Malawi ameapa kumaliza ufisadi serikalini na kujenga upya uchumi uliodorora baada ya kuapishwa Jumamosi kwa muhula wa pili kama rais wa taifa hilo la kusini mwa Afrika.

Mutharika, 85, alipata zaidi ya 56% ya kura mwezi uliopita, na kumshinda rais anayemaliza muda wake Lazarus Chakwera, 70, aliyepata 33% ya kura zilizopigwa.

Wapiga kura walimkataa Chakwera baada ya miaka mitano ya mgogoro wa kiuchumi unaozidi kuwa mbaya katika mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani.

Katika hotuba yake ya kuapishwa, alisema utawala wake unarithi nchi iliyo katika msukosuko wa kiuchumi.

Malawi inakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, gharama ya juu ya maisha, na ukosefu wa fedha za kigeni ambao umedumaza biashara na kusababisha uhaba wa mafuta, alisema.

"Hakuna pesa serikalini. Kukopa ni kiwango cha juu sana, na hakuna anayejua pesa zilizokopwa zimeenda wapi," alisema.

Lakini aliahidi maboresho, akisema: "Tutaiweka sawa nchi hii.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI