Header Ads Widget

RC SIMIYU APIGA KURA, AKIHAMASISHA USHIRIKI WA WANANCHI.

 

MKUU wa Mkoa wa Simiyu, AnaMringi Macha akiwaonyesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) kidole chake kilichopakwa wino mara baada ya kupiga kura Shule ya Sekondari Bariadi.


Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.


MKUU wa Mkoa wa Simiyu, AnaMringi Macha ameshiriki zoezi la kupiga kupiga kura katika kituo cha kupigia kura kilichopo Shule ya Sekondari Bariadi katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi na kuwataka wananchi kushiriki zoezi hilo ambalo linafanyika kwa amani na Utulivu.


Akizungumza mara baada ya kupiga kura, Macha amesema kuwa wapiga kura wanaojitokeza wamejiandaa vizuri na kwamba Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imeandaa Mazingira yanayowezesha wananchi kupiga kura bila foleni ndefu.


Amesema kuwa Mkoa wa Simiyu una vituo vya kupigia kura 2,950 kwa ajili ya kushughulikia wapiga kura zaidi ya Mil.1,222,000 na kwamba hali ya upigaji kura ni shwari, hakuna vurugu yoyote wala viashiria vya maandamano.


"tutaendelea kujitahidi kuhakikisha zoezi hili linaenda kwa amani, niwahakikishie Watanzania hakuna viashiria vyovyote au changamoto ya amani...kama kuna watu wanajiandaa kuleta fujo, nafasi hiyo haipo, tuendelee kutimizia Wajibu wetu wa kidemokrasia wa kuchagua viongozi" amesema Macha.




Naye Semeni kingi, ambaye ni mtu mwenye Ualbino ameipongeza Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kwa kuweka Mazingira mazuri ya Uchaguzi ikiwemo wenye ulemavu kupewa kipaumbele.



"nimetimiza jukumu langu kikatiba kupiga kura, nawaomba hawajafika kwenye vituo vya kupigia kura wafike ili wachague viongozi wanaowataka... Watu Wenye ulemavu wajitokeze kupiga kura sababu serikali imetuwekea Mazingira wezeshi ili kupiga kura" amesema Semeni. 


Mwisho.












Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI