Asema hali ya usalama mkoa Arusha ni Shwari na Salama
Awahimiza wananchi wenye sifa kujitokeza kutumia haki yao ya Kikatiba
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla mapema asubuhi ya leo Oktoba 29,2025 amewaongoza wananchi wa mkoa wa Arusha kupiga kura kwa kutimiza wajibu wake na kutumia haki yake ya Kikatiba ya kuchagua viongozikatiba ya kkuchagua viongozi.
CPA Makalla mara baada ya kukamilisha zoezi la upigaji kura kwenye Kituo chake cha AICC Hospitali Jijini Arusha, ameendelea kuwahakikishia wananchi wote kuwa hali ya usalama iko shwari na kuwataka wananchi wote wenye sifa kujitokeza kwa wingi ili kutimiza haki yako ya kikatiba ya kuchagua viongozi wao watakaowaongoza kwa kipindi cha miaka mitano.
Aidha, CPA Makalla ametumia muda huo kuwahamasisha wananchi wa Arusha wenye sifa kujitokeza kupiga kura huku akiwathibitishia wananchi wote kuwa, Tume imeweka utaratibu mzuri kwa kuwa na vituo vingi, ambavyo vinawezesha mpiga kura kutotumia muda mrefu kusimama kituoni.
"Mimi mwenyewe nimeshatimiza wajibu wangu, vituo tayari viko wazii, kuanzia saa 01:00 asubuhi mpaka saa 10:00 jioni, nimefurahi utaratibu ni mzuri hakuna foleni kubwa vituo ni vingi hivyo mtu akifika kituoni hatatumia muda mrefu, kila mtu atumie muda huo kwenda kwenye kituo alichojuandikisha" Amebainisha CPA Makalla.
MWISHO.







0 Comments