NA MATUKIO DAIMA MEDIA.
Zoezi la kupiga kura linaendelea kwa hali ya utulivu katika Kata ya Kirumba, Halmashauri ya Ilemela, jijini Mwanza, huku wananchi wakijitokeza kwa wingi kutekeleza haki yao ya kikatiba.
Wananchi wameonekana wakiwa katika mistari wakiingia vituoni mapema asubuhi, wakisubiri kwa utulivu nafasi yao ya kupiga kura. Maafisa wa Tume ya Uchaguzi wamesema maandalizi yamekuwa mazuri na vifaa vyote vya kupigia kura vimefika kwa wakati.
Wamewataka wapiga kura kuendelea kujitokeza kwa amani na kufuata maelekezo yanayotolewa na wasimamizi wa vituo, ili kuhakikisha zoezi hilo muhimu kwa demokrasia ya nchi linafanikiwa kwa utulivu na uwazi.
MWISHO


.jpeg)




0 Comments