Na mwandishi wetu
Zikiwa zimesalia siku 9 ili wananchi waingie kwenye chumba Cha kupigia kura kumpata Rais, Wabunge na madiwani katika uchaguzi mkuu wa Mwaka huu, Jeshi la Polisi mkoani Njombe limeonya wanaotumia vibaya Mitandao ya Kijamii kutaka kuvuruga zoezi Hilo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Mahamoud Banga mbele ya vyombo vya habari anasema wanaendelea na doria ya kitandaoni ili kubaini yeyote anayetumia vibaya Mitandao hiyo kuchochea chuki kuelekea Uchaguzi mkuu.
Aidha Kamanda Banga amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo kwani ulinzi utaimarishwa katika Maeneo yote
Baadhi ya wananchi mkoani Njombe Wamesema wapo Tayari kushiriki katika uchaguzi huo huku wakitaka Mitandao ya Kijamii isitumike vibaya.
0 Comments