Header Ads Widget

TCU YAVIELEKEZA VYUO VIKUU KUZINGATIA UFUNDISHA UNAOLENGA UMAHIRI

 



Na Lilian Kasenene,Morogoro

Matukio DaimaApp 

TUME ya vyuo Vikuu nchini (TCU) imevielekeza vyuo hivyo kuzingatia ufundishaji unaolenga ujuzi, umahiri, maarifa na mahitaji ya soko la ajira.

Akimwakilisha katibu mtendaji wa TCU Profesa Charles Kihampa,

mkurugenzi wa Ithibati Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Dk Telemu Kassile, alisema hayo mkoani Morogoro kwenye warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo Wahadhili, wanataaluma na viongozi katika ngazi za utawala Chuo Kikuu Cha Sokine Cha Kilimo SUA, mafunzo yenye lengo la kuwapa mbinu mbalimbali za namna ya kufundisha mitaala iliyofanyiwa marejeo baada ya sera ya Elimu ya mafunzo ya Mwaka 2014 kufanyiwa mapitio na kutoa toleo la Mwaka 2023.

Mkurugenzi wa ithibati TCU Dk Telemu Kassile akifungua mafunzo

Dk Kassile ufundishaji huo ni ili kwenda sambamba na mabadiliko ya mitaala na sera zilizofanyika

Sera hiyo imesisitiza wahitimu kuwa na ujuzi na Tume kama wasimamizizi wa vyuo vikuu nchini ilitoa maelekezo kuhuwisha mitaala yao na vile vinavyoandaa mitaala mipya kuandaa itakayowapa wahitimu ujuzi wa kujiajiri ama kuajiriwa pindi watakapomaliza masomo yao.

Aidha alisema TCU imekuwa na mafunzo kwa wanataaluma ambao si walimu ambao wanaajiriwa vyuoni, ambapo kwa miaka minne iliyopita tume imeweza kuwajengea uwezo wanataaluma 800 kutoka vyuo vikuu vya umma na binafsi ambao sio wanataaluma kwa mafunzo.

Dk Kassile alisema mabadiliko yalivyofanyika hayapunguzi ubora na ndo maana tume imetoa ithibati na kuhuwisha ithibati ya mitaala kwa sababu imezingatia mahitaji ya soko na kwamba wanafunzi wanapokuwa wanasoma vyuoni wanasoma programu kwa ajili ya kwenda kuhudumu katika maeneo tofauti hivyo matarajio wanapotoka wawe na ujuzi wa kutosha na maarifa..

Akaeleza namna walivyojipanga kuongeza ushirikiano baina ya Vyuo Vikuu Tanzania na taasisi za kimataifa na kwamba vyuo vinaruhusiwa kuingia mashirikiano na taasisi yoyote kitaifa na kimataifa, ikiwemo sekta za viwandaz vyuo na maeneo mengine kama namna ya kutoa maarifa.

Alisema Chuo Kikuu Cha Sokine Cha Kilimo SUA kwa ushirikiano na taasisi ya REFORUM itasaidia wahitimu kuwa na ujuzi mkubwa na kwamba wamekuwa wakitengenezwa pia kwa ajili ya soko la nje.

Naibu makamu mkuu wa chuo kikuu cha sokoine cha kilimo SUA,upande wa Taaluma Prof Maulid Mwatawala alizungumzia maandalizi waliofanya mpaka Sasa kuwa wamefanya mapitio ya mitaala yake yote kutoka Ile iliyokuwepo ili kuifanya iwe ya Elimu kwa vitendo zaidi na wataanza kuyaendesha Novemba Mwaka huu wa 2025 vyuo vifakapounguliwa.

Prof Mwatawala alisema kwa kuzingatia hilo wameanza na mafunzo kwa walimu kwa kuwajengea uwezo kwa sababu wanahitaji stadi mahususi ili kuendana na mitaala, lengo ni kuhama kutoka mwanafunzi anafahamu nini kwenda mwanafunzi anaweza kufanya nini ili kuendana na soko lililopo.

Pia alisema SUA itaboresha na mkazo mkubwa utakuwa kwenye stadi na utoaji wa mafunzo utabadilika mfano kwa Sasa watakuwa na wale wanaotaka kwenye viwanda, na maeneo mengine ya kazi ambao wana uzoefu lakini si walimu wa Chuo kikuu na ufundishaji huo utaenda kidigitali zaidi.

"Kwa hiyo sehemu kubwa ya mafunzo mwanafunzi ataweza kujifunza mwenyewe na kushirikiana na wenzie, sio ule mtindo wa zamani na Sasa tumebadili mifumo wa mafunzo kwa vitendo ambao utakuwa wa semester nzima ili ajifunze stadi za kazi na Mazingira ili akimaliza aingie kazini Moja kwa Moja ikiwa kwa kujiajiri au kuajiriwa,"alisema.


Naibu huyo makamu wa SUA alisema kupitia mradi wa HEET wameweza kujenda miundombinu ya kufundishia, na kwamba kwa wanataalumu kwa kipindi Cha miaka mitatu wameweza kuajiri walimu 150 wapya.

Afisa programu, wahitimu na mabadiliko ya kitaaluma, RUFORUM Emmanuel Okalany, alibainisha changamoto ya vijana wengi wa vyuo vikuu kuhitimu na kukosa ajira ni kutokuwa na kutokuwa na ujuzi wa kutosha na kwamba kwa sasa kinachotakiwa kuendelea kufanyika ni  kubadilika kwa mtazamo wa Afrika kwa kizazi kilichopo na kijacho.

Okalany alisema kupitia jukwaa maalumu linaloundwa na vyuo vikuu 175 katika nchi 40 za bara la Afrika, linalolenga kujenga uwezo katika sekta ya kilimo, jukwaa hilo linasaidia vyuo vikuu wanachama kufundisha Vijana kuwaeleza changamoto za ajira baada ya kuhitimu na namna ya kukabiliana nazo.

"Tatizo lililopo ni namna gani Vijana wanapataje ajira baada ya kuhitimu masomo yao, Sasa wanataaluma na vyuo vikuu kubadili mtazamo na kuondokana na tamaduni za zamani na kuwafundisha kukabiliana na changamoto zote wakiwa bado wako vyuoni,"alisema

Nae naibu makamu mkuu wa chuo kikuu cha sokoine,mipango,fedha na utawala Prof Amandus Muhairwa, alisema muda wa kulalamika umekwisha kwa sababu rasilimali zote zipo na wakati wa Sasa ni kutenda na inawezekana Kila mmoja akatimiza wajibu wake.

Prof Muhairwa alisema katika mafunzo wataalamu wafanye kile wanacho kiongea kwa vitendo, ni kuwasukuma wataalamu kuwapeleka wanafunzi katika kutenda zaidi ili mwanafunzi aone matokeo.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI