Header Ads Widget

NJALU AOMBA KURA AKIWAAHIDI WANANCHI USHIRIKIANO




Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.


MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Itilima kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Njalu Silanga amewataka wananchi kuchagua viongozi wanaotokana na CCM ili waendelee kuchapa kazi, baada ya kumaliza miaka mitano (2020/2025) ya Uongozi kwa Mafanikio makubwa.


Akizungumza kwenye Mikutano ya kampeni katika vijiji vya Mwaogama, Mwanhunda, Mwabuligu na Isengwa wilayani Itilima, Njalu amewashukuru wananchi kwa kumpatia ushirikiano yeye na viongozi wengine ndani ya miaka mitano.


"Miaka mitano tumeimaliza kwa mafanikio makubwa, kila tulichoahidi tumetekeza...ni kwasababu ya ushirikiano na upendo wenu Wanaitilima kwangu na Mapenzi Makubwa ya Mama Samia Kwetu" amesema Njalu na kuongeza.


"Leo nimerudi tena kwenu nikiwa na ujasiri kusema kwamba tunaenda kufanya makubwa zaidi kwa sababu changamoto za maeneo yetu sihitaji kusimuliwa bali nazijua kwa kuziishi na kujionea mwenyewe."


Njalu amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi Oktoba 29, 2025 kumpigia kura nyingi Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mbunge  (Njalu) na Madiwani wote wa CCM ili kazi ya ujenzi wa Itilima iendelee.


Mwisho.










Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI