Na Shemsa Mussa -Matukio Daima
Kagera.
MV Mwanza imefanya safari ya matazamio Kwa lengo la kujihakikishia ubora na usalama Wa meli hiyo ili kuwa tayari Kwa Kuanza safari yake rasmi.
Safari ya matazamio ya meli ya MV Mwanza imeanza rasmi Leo ikihusisha abilia na mizigo ikitokea Mkoani mwanza kuja bandari ya Bukoba kupitia bandari ya kemondo ikiwa ni hatua ya pili ya majaribio ya Ukamilifu Wa ujenzi wa meli hiyo.
Akizungumza baada ya meli hiyo kutia nanga Katika bandari ya Bukoba wakala Wa meli Tanzania (TASAC)Mhandisi Said kaheneko kaimu meneja Wa usajili na ukaguzi,amesema baada ya safari ya majaribio iliyofanyika hivi karibuni walibaini baadhi ya changamoto ikiwemo Chombo hicho kutoa sauti kubwa zaidi.
" Jaribio lile la mwanzo Tulibaini tatizo kidogo la meli kutoa sauti ya juu pia tukabaini sababu kubwa kuwa ni meli hiyo ilikuja bila mizigo Wala abilia tulikuwepo sisi wataalamu tu na tukaona tufanye jaribio la pili ili tuweke mizigo na abilia angau nusu ya uwezo Wa kile inachotakiwa kubebwa ili tujilidhishe zaidi amesema Mha,Kaheneko"
Amesema meli hiyo imeanza safari kutoka mwanza majira ya saa 4 usiku na kufika bandari ya kemondo saa 11 alfajir na kutia nanga katika bandari ya Bukoba majira ya saa 1 asubuhi huku ikiwa imebeba abilia 414 na mizigo ya tani 78.6 ikiwa uwezo Wa kubeba Tani 400 na abilia 1200.
amesema baada ya majaribio hayo watatoa kubali rasmi Kwa ajili ya kuwa tayari kuoanga safari rasmi.
Naye Afisa uhusiano kutoka Katika kampuni ya meliTASHICO Bw,Abdulrahmani Salim,amasema Chombo hicho Cha usafiri majini Bado hakijaanza safari rasmi na kuwa safari ya Leo umekuwa safari ya matazamio kuwa meli hiyo imekuja na watu na mizigo na itarudi na abilia na mizigo,huku akiwakaribisha Wananchi kujitokeza kuchangamkia fursa hiyo huku wakisubilia ratiba rasmi.
0 Comments