Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Zaidi ya wanachama 200 wa Chama Cha ACT Wazalendo wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi wakieleza kuridhishwa na utendaji wa Rais Samia Suluhu Hassan na serikali.
Wanachama hao wamepokewa na Mwenyekiti wa CCM mkoa Kigoma, Jamal Tamim katika mkutano wa hadhara wa kampeni ya Mgombea ubunge wa CCM jimbo la Kigoma Kusini uliofanyika kijiji cha Ilagala wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.
Tamim amewapokea wanachama hao kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye tarehe 14 akiwa kwenye mkutano wa kampeni kwenye viwanja vya Katosho Manispaa ya Kigoma Ujiji alimpokea Mratibu wa kampeni wa ACT Wazalendo mkoa Kigoma,Saidi Bakema ambaye alisemaa kuwa alikuwa na kundi la watu Zaidi ya 200 ambao wameongozana nao.
Mwenyekiti wa CCM mkoa Kigoma akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Ilagala wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma ambapo alipokea wanachama 200 wa Chama Cha ACT Wazalendo
Katika mkutano huo Raisi Samia alimpokea Kiongozi huyo na kuahidi kuwa atatuma wasaidizi wake kuwapokea wanachama na viongozii wengine wa chama hicho na ndiyo Mwenyekiti huyo amewapokea wanachama hao katika mkutano huo wa Ilagala.
Akiwapokea Wanachama hao Mwenyekiti huyo wa CCM mkoa Kigoma alisema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amefanya makubwa ya maendeleo kwa wananchi wa mkoa Kigoma hivyo wanachama hao wanayo sababu ya kuunga mkono na kuunga juhudi zinazofanywa na kiongozi huyo.
Mwenyekiti wa CCM mkoa Kigoma Jamal Tamim akipokea kadi za wanachama wa Chama Cha ACT Wazalendo waliojiunga na CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Ilagala wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma ambapo alipokea wanachama 200 wa Chama Cha ACT Wazalendo
0 Comments