Header Ads Widget

BALOZI DKT. PINDI CHANA AJITOKEZA MAPEMA KUPIGA KURA IRINGA

 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA.

IRINGA.Balozi Dkt. Pindi Chana amekuwa miongoni mwa viongozi wa serikali waliojitokeza mapema leo kushiriki zoezi la kupiga kura, akitimiza haki yake ya Kikatiba.

Dkt. Chana amepiga kura katika kituo cha Chuo cha Afya, kilichopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, ambapo shughuli ya upigaji kura imeanza kwa utulivu na amani.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya zoezi hilo Dkt. Chana amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao hiyo muhimu, akisisitiza umuhimu wa kudumisha amani wakati wote wa mchakato wa uchaguzi.

Hata hivyo, mpaka muda wa saa tatu asubuhi, idadi ya wapiga kura waliokuwa wamejitokeza katika kituo hicho bado haikuwa ya kuridhisha, huku maafisa wasimamizi wa uchaguzi wakiendelea kuhimiza wananchi kufika vituoni mapema kabla ya muda wa kufunga vituo.

Zoezi la upigaji kura linaendelea katika vituo mbalimbali vya mkoa wa Iringa na maeneo mengine nchini, likiendelea kwa utulivu mkubwa.

MWISHO.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI