NA MATUKIO DAIMA MEDIA
IRINGA.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kwa tiketi ya Chama cha mapinduzi(CCM) Fadhili Ngajilo, ameungana na Watanzania wengine kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu unaoendelea leo nchini kote,Kama sehemu ya kutimiza haki yake ya Kikatiba.
Ngajilo amepiga kura katika Kituo cha VETA, Mjini Iringa, na kueleza kuwa ameridhishwa na hali ya utulivu iliyopo wakati wa zoezi hilo.
"Zoezi la kupiga kura limeendeshwa kwa amani na utulivu mkubwa, nawaomba wananchi waendelee kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mchakato huu muhimu kwa mustakabali wa taifa"alisema
MWISHO






0 Comments