NA MATUKIO DAIMA MEDIA.
MAFINGA.Mratibu wa kampeni za Chama cha Mapinduzi Nyanda za juu kusini na Mjumbe wa kamati kuu ya Taifa ya Chama cha mapinduzi MCC, Salim Abri Asas amewaomba wananchi kujitokeza kwa amani na utulivu kwenda kupiga kura tarehe 29 oktoba.
MCC Salim amesema hayo wakati akifunga kampeni jimbo la Mafinga mjini na kuomba kura za kutosha kwa Dkt Samia,wabunge na Madiwani wa chama cha Mapinduzi.
MCC Salim amesema kuwa mtu anapoenda kupiga kura atoke na amani huku roho yake ikiwa imetulia apige kura na kurudi nyumbani kupumzika
"Msihofu na chochote wala asiwatishe yeyote nendeni mkapige kura na muwe na amani na utulivu, uchaguzi wetu ni wa amani na hakuna baya lolote litakalotokea"alisema
Akimnadi Mgombea Ubunge wa jimbo la Mafinga Mji Dickson Lutevele alisema ni mtu ambaye akipewa ushirikiano jimbo hilo litapata maendeleo hivyo wampigie kura nyingi za ndio ili aweze kuwatumikia.
"Ili Mbunge afanye vizuri lazima awe na madiwani ambao wanatokana na chama cha mapinduzi pia nawaomba muwapigie kura ili iwe rahisi mbunge kufanya kazi akiwa bungeni"alisema
"Niwasisitize najua wote hapa mnaelimu ya kupiga kura hivyo niwaombe wote mjitokeze kupiga kura, kutakuwa na ulinzi wa kutosha na hatutakuwa na ghasia yeyote, kwa kuwa vyombo vya ulizi na usalama vimetuhakikishia ulinzi na usalama wa kila mwananchi"alisema
Akizungumza Mgombea Ubunge jimbo la Mafinga Mjini Dickson Lutevele alisema kuwa amefanya mikutano isiyopungua 35 na kukutana na wananchi wasiopungua 12,000 na kutembea katika makundi maalum mbalimbali.
Alisema kuwa wana Mafinga wanahitaji maji, barabara, kuwezeshwa kiuchumi,wanahitaji watoto wasome bure, vijana na akina mama na watu wenye ulemavu wapate mikopo,na kuwaendeleza wasanii na kuimarisha michezo.
"Ili yotye hayo yafanyike tumekubaliana na wanamafinga kuwa oktoba 29 tunakwenda kutiki kwa Dkt Samia,Mbunge na madiwani wake ili kuweza kufanya maendeleo kwa kushirikiana, tuwe na uongozi bora, na nchi lazima iwe na amani"alisema
Lutevele alisema kuwa siku ya jumatano saa mbili kamili asubuhi wamekubaliana watajaa katika vituo vya kupigia kura na baada ya kupiga kura watarudi nyumbani kupumzika na hakuna haja ya maandamano.
"Kote nilikopita katika kata 9 na matawi yake tatizo kubwa ni ofisi za chama za mapinduzi kuwa chakavu na wengine hawana kabisa,hivyo nakuomba mlezi wetu MCC Salim Asas ile ahadi ambayo umeniahidi kuwa ujengaji wa kata katika wilaya ya Mufindi utakapoanza naomba na mimi nikuunge mkono, nitachanga tani 30 za cimenti "alisema
MWISHO.

.jpeg)


.jpeg)




0 Comments