Na Frank Vegullah, Matukio Daima Media Kalenga
Baada ya mfululizo wa siku 42 za kampeni hatimae Jumapili hii october 26 Mgombea ubunge wa Jimbo la Kalenga Mh.Jackson kiswaga amehitimisha kampeni zake rasmi katika viwanja vya zahanati vilivyopo kata ya Magulilwa
Kiswaga ambae anaomba ridhaa ya kuwaongoza wananchi wa jimbo la Kalenga kwa kipindi cha miaka mingine mitano, alianza kampeni zake rasmi tarehe 13 ya mwezi septemba katika kata ya Nzihi na katika kuhitimisha hii leo alipata kuzungumza na mamia ya wananchi wa kata ya magulilwa ambao kwa kauli moja wamemuahidi kumpa kura za kishindo ifikapo OKTOBA 29 Ambayo ndio siku rasmi ya uchaguzi mkuu
Mkutano huu wa tamati ya kampeni ulishuhudia pia uwepo wa wagombea wote wa udiwani wa kata za Jimbo la Kalenga akiwemo mwenyeji Boazi mbilinyi ambae ni mgombea mteule udiwani Ccm kata ya Magulilwa,pia umehudhuriwa na viongozi wa chama kata ya magulilwa,wazee wa kimila,pamoja na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa vijijini Ndugu Constatino Kihwele ambae ndie alikuwa mgeni rasmi
Hii imekua ni kilele cha safari ya kampeni za Mbunge mteule Jakson kiswaga ambae amekutana na wananchi wa Jimbo la kalenga kwa ajili ya kuhitimisha rasmi kampeni na kuwasihi wakazi wa jimbo hilo wamchague tena kuwa Mbunge wao, pamoja na kuwapigia kura wagombea wa Udiwani wa CCM na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kiswaga katika Kampeni za kuhitimisha hii leo pamoja na zile za kijiji Kwa kijiji na kata Kwa kata ameendelea kusisitiza kuwa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo katika sekta za maji, barabara, afya, elimu na nishati, na kwamba utekelezaji wa Ilani ya CCM 2025–2030 utaongeza kasi ya maendeleo hayo.
Iwapo atachaguliwa tena kiswaga ataingia katika awamu yake ya pili ya ubunge, akiahidi kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyoanzishwa na kutekelezwa katika kipindi cha kwanza(2020-2025) iikiwemo miradi ya maji,umeme,miundombinu ya Barabara,kilimo,elimu na Afya.







0 Comments