Header Ads Widget

MBEYA DC YAONGOZA KIKANDA MWENGE WA UHURU 2025.

 

Na Josea Sinkala, Mbeya.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Bi. Erica E. Yegella, amepokea zawadi ya ushindi wa kwanza kwa niaba ya Halmashauri ya wilaya ya Mbeya baada ya Halmashauri hiyo (Mbeya DC) kuibuka kinara kikanda.

Hata hivyo katika ngazi ya Kitaifa Halmashauri ya wilaya ya Geita (Geita DC) ndio imetangazwa kuwa mshindi wa kwanza.

Huu ni ushahidi wa jitihada madhubuti za uongozi na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya katika kuleta maendeleo kwa kudumisha ushirikiano na utendaji kazi miongoni mwao na wananchi kwa ujumla wake.

Pichani mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya Erica Yegella akiwa na mkuu wa wilaya ya Mbeya Mhe. Solomon Itunda baada ya kupokea zawadi ya ushindi kwa niaba ya Halmashauri ya Mbeya ambapo shughuli za mwenge zimemalizika kwa kuzimwa mwenge wa uhuru katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Oktoba 14, 2025.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI