Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), William Vangimembe Lukuvi, ameshiriki ibada maalum ya kumuombea Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Francisko wa Asizi Mwanjelwa, Jijini Mbeya, na kuongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Mbeya, Mhashamu Gervas Nyaisonga.
Katika maombi hayo, waumini waliendelea kumkumbuka Mwalimu Nyerere kwa mchango wake mkubwa katika msingi wa umoja, amani na maendeleo ya taifa la Tanzania.
0 Comments