Na matukio daima media
Mgombea Ubunge kupitia chama cha mapinduzi CCM Jimbo la Mchinga Mkoani Lindi Leo amehitimisha kampeni zake Kwa kunadi Sera za Chama hicho huku akiwasihi wananchi wa Jimbo hilo kuchagua viongozi wanaotokana na CCM kwani kina Ilani inayotekelezeka
Ni tamati ya kampeni za Rais wabunge na Madiwani zikihitimishwa hapa Katika Kata ya Nangaru Manispaa ya Lindi ambapo Mama Salma Kikwete anawaahidi wananchi hawa kushirikiana nao Katika shughuli mbalimbali za Maendeleo ikiwemo ujenzi wa Kituo cha Afya Katika Tarafa hiyo
Amesema chama cha mapinduzi kupitia Ilani ya ya Uchaguzi 2025/2030 inatambua tatizo hilo na ni miongoni mwa mambo yatakayoenda kufanyiwa kazi
Salum Ng'ondo Ni Mgombea udiwani wa Kata hiyo ya Nangaru Akatumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi wa Kata hiyo kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 29 oktoba kwenda kukipigia Kura chama cha mapinduzi
Kampeni hizo zilizoanza takriban miezi mwili iliyopita zimekuwa zikipokelewa kwa hamasa Katika vijiji na Kata za Jimbo Hilo la Mchinga ambapo wananchi wameonesha matumaini kwa Mgombea huyo wa Ubunge





0 Comments