Na Shemsa Mussa -Matukio Daima
Hospitali ya rufaa ya Mkoa,Bukoba kupitia kitengo Cha macho kwa kushirikiana na shirika la KCCO imeanza zoeli la Uchunguzi Wa awali wa magonjwa ya macho ikiwa zoezi Hilo linafanyika Bure Kwa Wananchi Mkoani humo.
Akizungumza ofisini kwake Mganga Mfawidhi Wa Hospitali hiyo Dkt Museleta Nyakiroto,amesema Kila ifikapo Alhamisi ya pili ya mwezi Octoba Kila mwaka dunia nzima uadhimisha siku ya afya ya macho kwa lengo la kuongeza uelewa Kwa jamii kuhusu umuhimu Wa kutunza macho.
Dkt Nyakiroto,amesema kuwa zoezi Hilo litafanyika kuanzia Tarehe 8 Octoba Hadi 10 Mwaka huu kuanzia saa 1 asubuhi Hadi saa 9 mchana na kusema kuwa wagonjwa watakaobainika kuwa na tatizo la macho linalohitaji matibabu, kuwa wataingizwa Katika utaratibu Wa Kupata matibabu hospitalini hapo.
Amesema tafiti zinaonesha zaidi ya asilimia 75 ya matatizo ya macho yanaweza kuzuilika na kupatiwa matibabu endapo yatagundulika mapema ,pia amewakalibisha Wananchi Wa Mkoa huo na Maeneo jirani kushiriki Katika zoezi Hilo ili kuwa na jamii yenye uoni Bora.
0 Comments