WANANCHI wa kata ya Mlenge jimbo la Isimani wamejitokeza kwa wingi leo kusikiliza sera za mgombea ubunge wa jimbo hilo Wiliam Vangimembe Lukuvi.
Lukuvi amekuwa akipata mapokezi makubwa kwenye mikutano yake kila kata anayopita kuomba kura za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ,kura zake mbunge na kura za madiwani wa kata zinazounda jimbo la Isimani .
Akiwa katika mikutano ya kampeni Lukuvi amewaomba wananchi kuendelea kujenga imani na serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwani ni serikali yenye mapenzi ya kweli ya kuleta maendeleo na ndio maana wanashuhudia miradi mingi ikitekelezwa .
Lukuvi alisema ili miradi hiyo na mingine izidi kutekelezwa wananchi wanapaswa kutoa kura za kishindo oktoba 29 kwa Mgombea urais wa CCM Dkt Samia ,mbunge na madiwani wote wa CCM ili waweze kusimamia ilani ya CCM.
0 Comments