Header Ads Widget

LUKUVI AHITIMISHA KAMPENI, AWAOMBA WANANCHI WAMCHAGUE DKT. SAMIA NA CCM KWA MAENDELEO ZAIDI


Na Matukio Daima Media, ISMANI 

Mgombea ubunge wa Jimbo la Isimani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), William Lukuvi, amewataka wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 kupiga kura za ndiyo kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, wagombea ubunge na madiwani wa CCM, ili kuendeleza kasi ya maendeleo iliyoanza chini ya serikali ya chama hicho.

Akihitimisha kampeni zake katika mkutano uliofanyika kijijini Idodi, kata ya Idodi, wilayani Iringa, Lukuvi alisema kuwa CCM ndiyo chama pekee chenye ilani na dira ya maendeleo inayoonekana kwa vitendo.

 “Awamu ya uongozi wangu uliopita tumetekeleza miradi mikubwa kama ujenzi wa vituo vya afya, mifereji ya umwagiliaji, shule za sekondari na barabara zinazounganisha vijiji,” alisema Lukuvi.

Alibainisha kuwa barabara kubwa inayopita Tungamalenga imekuwa kichocheo kikubwa cha uchumi wa eneo hilo, huku akiahidi kuwa kura nyingi kwa Dkt. Samia zitaharakisha kukamilika kwa mradi wa maji na kuimarisha kilimo cha umwagiliaji.



Akizungumzia sekta ya elimu, Lukuvi alisema serikali ya CCM inaendelea kuboresha mfumo wa elimu kwa kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu endelevu kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha 12 bila vikwazo.

 “Watoto wa Magogolo na maeneo mengine hawatabaki nyuma. Watasoma hadi kidato cha 12, watafundishwa ujasiriamali na stadi za kilimo ili waweze kujitegemea. Hakutakuwa na ndoa za utotoni wala kukatishwa masomo,” alisema.

Aliongeza kuwa mfumo huo wa elimu unaolenga ujuzi na ubunifu utaondoa dhana kwamba kila kijana anapaswa kuajiriwa na serikali.

 “CCM inaamini katika elimu ya kujitegemea. Vijana watafundishwa namna ya kujiajiri kupitia kilimo, biashara na teknolojia, ili wawe sehemu ya uchumi wa taifa,” alisisitiza.

Lukuvi aliwahimiza wananchi kuchagua CCM kwa sababu ni chama kilichojenga misingi ya amani, umoja na maendeleo endelevu nchini.


 “CCM imeleta miradi ya maji, afya, barabara, elimu na umeme vijijini. Dkt. Samia ameonyesha uongozi wa mfano kwa kuwekeza kwenye miradi mikubwa ya kimkakati kama reli ya kisasa (SGR), nishati safi, na kuinua wanawake na vijana kiuchumi,” alisema Lukuvi.

Alisisitiza kuwa kura kwa Dkt. Samia na wagombea wa CCM ni kura za kuendeleza amani, maendeleo na ustawi wa Watanzania wote.

“Tukichagua CCM, tunachagua maendeleo yanayoonekana, tunachagua utulivu, na tunachagua mustakabali bora wa watoto wetu,” alisema kwa msisitizo.


cWHsI6fi58N8P5W1kPp7OZwlA9ZF53UBnYsRwBYcQtA_W7OyRXbXyppo0KlAB0-xVKtlzOPZ6Q1zyy72lqkM1s7QLOGvkUTCaYWwLeWEsb1Rwyby37z1arJZBsIeX7CLDasjf-J2LME2cTaMhwPUNGpslpZcTsTn0bDtYaz3dJUSBj7xQu88/s1600/141904.jpg" style="display: block; padding: 1em 0; text-align: center; clear: right; float: right;">

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI