Na Hadija Omary
Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT ) Mkoa wa Lindi Mwalimu Halima Liveta anawataka walimu wa Mkoa wa Lindi kupuuza taarifa za upotoshaji zinazosambaa katika mitandao ya kijamii zinazoeleza walimu kutoshiriki uchaguzi mkuu wa oktoba 29, 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Leo oktoba 27/2025 mwalimu liveta Amesema chama kinakanusha taarifa zinazoendelea Katika mitandao ya kijamii ikihamasisha walimu kutoshiriki shughuli za Uchaguzi kwa mujibu wa Sheria, kanuni na taratibu za Serikali.
"Chama kinatoa Rai kwa walimu wote kupuuza taarifa hizo kwani hazina ukweli bali zinalenga kutuletea taaluki uzushi na uchonganishi"
Amesema chama kinasisitiza kama Raia wengine wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania wanahaki ya kikatiba ya kushiriki Katika zoezi la kupiga Kura





0 Comments