Na Josea Sinkala, Mbeya.
Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Mbeya vijijini Gideon Mapunda, amefunga mafunzo ya wasimamizi wa uchaguzi na makarani ambayo yamefanyika katika mamlaka ya mji mdogo wa Mbalizi wilayani Mbeya.
Katika mafunzo hayo, msimamizi wa uchaguzi Mbeya vijijini ametoa maagizo mahususi kwa wahusika wote katika kusimamia na kufanikisha zoezi la uchaguzi bila vikwazo vyovyote wakiwemo wasimamizi wasaidizi na makarani kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuzingatia sheria, miongozo, kanuni na maadili wanayoyakiwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha haki inatendeka.
Akizungumza baada ya mafunzo hayo ya siku mbili, Mapunda amesema hana mashaka kuwa uchaguzi huo utafanyika kwa haki na kuwataka wananchi katika jimbo la Mbeya vijijini kujitokeza kutimiza haki yao ya kikatiba kwenda kupiga kura kuchagua viongozi wanaowataka kwa maendeleo yao.
Pamoja na hayo amewashauri wananchi kuwa ni muhimu wakishapiga kura warudi majumbani kusubiri matokeo badala ya kubaki vituoni.
Nao baadhi ya washiriki akiwemo bi. Amina Munisi msimamizi msaidizi katika moja ya vituo huko katika kata ya Igale, wameahidi kwenda kusimamia viapo vyao kufanya kazi kwa weledi ikiwemo kuhakikisha kila mwananchi anayefika kituoni anapiga kura.





0 Comments