NA MATUKIO DAIMA MEDIA.
NACHINGWEA.Mgombea Ubunge wa Jimbo la Nachingwea Mkoani Lindi anewaongoza wananchi wa Jimbo Hilo kushiriki zoezi la upigaji wa Kura Katika Uchaguzi Mkuu wa kuchagua Rais, wabunge na Madiwani uliofanyika Leo Nchi Mzima
Liwaka ameshiriki zoezi hilo Katika kituo cha kupiga Kura cha matangini Kata ya Nangoe Wilayani Nachingwe ambapo akizungumza mara baada ya kupiga Kura Liwaka amewasisitiza wananchi kuendelea kujitokeza Katika vituo vya kupigia Kura ili kutimiza wajibu wao wa kidemokrasia
Msimamizi wa Uchaguzi wa Kata hiyo Nangoe ally mkitage Amesema Katika vituo Tisa vya Kata hiyo Jumla ya wapiga Kura 3192 wamejiandikisha kupiga Kura Katika Kata hiyo huku akileza Hatua za Awali kwa kabla ya kushiriki kupiga Kura
Baadhi ya wapiga Kura wamepongeza utaratibu mzuri WA kupiga Kura uliweka na tume
MWISHO.







0 Comments