Ethiopia imeishutumu Eritrea kwa kujiandaa kuanzisha vita dhidi yake kwa kushirikiana na kundi la upinzani, katika ishara ya hivi punde ya kuongezeka kwa mvutano kati ya majirani hao wawili kuhusu udhibiti wa Bahari ya Shamu.
Tuhuma za Ethiopia zimo katika barua iliyotumwa na Waziri wake wa Mambo ya Nje Gedion Timothewos kwa mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, akionya kwamba njama hiyo imekuwa "dhahiri zaidi katika miezi michache iliyopita".
Eritrea bado haijatoa maoni yoyote kuhusu barua hiyo, lakini uhusiano wake na Ethiopia umezidi kuwa mbaya katika miezi ya hivi karibuni.
Ethiopia imekuwa ikikusanya usaidizi ili kurejesha ufikiaji wa Bahari ya Shamu, na kusababisha hofu nchini Eritrea ilipochukua udhibiti wa ukanda wa pwani wakati wa uhuru mnamo 1993.
Ikiwa madai ya Gedion ni ya kweli, ina maana kwamba Eritrea inaendesha vita vya wakala dhidi ya serikali ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, ili kuizuia isifanye uvamizi wa kijeshi nchini Eritrea ili kukamata bandari zilizo kando ya Bahari ya Shamu.
Ethiopia na Eritrea zilipigania udhibiti wa mji wa mpaka wa Badme kutoka 1998 hadi 2000, na kusababisha vifo vya makumi ya maelfu ya watu.
Baada ya Abiy kuchukua madaraka mwaka wa 2018, alimaliza mvutano kwa kujenga muungano imara na Rais wa Eritrea Isaias Afwerki.
Katika barua hiyo iliyoonwa na shirika la habari la AFP, Gedion alidai kwamba Eritrea na kundi lenye msimamo mkali la Tigray People's Liberation Front (TPLF) walikuwa "wakifadhili, wakihamasisha na kuongoza makundi yenye silaha" katika eneo la Amhara nchini Ethiopia, ambako wanamgambo wanaojulikana kama Fano wamekuwa wakipambana na serikali ya shirikisho.
0 Comments