Cristiano Ronaldo ameichezea Ureno mara 223
Cristiano Ronaldo ametajwa kuwa mchezaji bilionea wa kwanza katika soka, kwa mujibu wa chombo cha habari cha masuala ya fedha, Bloomberg.
Ripoti juu ya mabilionea ya Bloomberg, ambayo inawafuatilia watu matajiri zaidi duniani kulingana na thamani yao halisi, imepima utajiri wa mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 40 na Al-Nassr kwa mara ya kwanza.
Tathmini hiyo inazingatia mapato ya kazi, uwekezaji na matangazo na inasema thamani halisi ya Ronaldo ni dola bilioni 1.4 (£1.04bn).
Inasema alipata zaidi ya dola milioni 550 (£410m) kama mshahara kati ya 2002 na 2023, na mapato yake yaliyoripotiwa kupitia mikataba na ufadhili, ikiwa ni pamoja na mkataba wa muongo mmoja na Nike wenye thamani ya karibu dola milioni 18 (£13.4m) kwa mwaka.
Ronaldo alipojiunga na Al-Nassr kwenye Ligi ya Saudia mwaka 2022 aliripotiwa kuwa mchezaji anayelipwa vizuri zaidi katika historia ya soka na mshahara wa mwaka wa pauni milioni 177.
Mkataba wake ulipaswa kumalizika Juni 2025 lakini alitia saini mkataba mpya wa miaka miwili - unaoripotiwa kuwa na thamani ya zaidi ya dola milioni 400m (£298m) - ambao utamweka katika klabu hiyo hadi atakapo timiza miaka 42.
0 Comments