Header Ads Widget

DKT.MWINYI NA MAMA MARIAM MWINYI WASIMAMA NJIANI KUNUNUA MABUNGO


Na matukio daima media

 Mgombea wa nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akiwa ameambatana na mke wake Mama Mariam Mwinyi, wamesimama njiani kununua matunda aina ya Mabungo wakitokea Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, baada ya mkutano wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), katika mwendelezo wa kampeni zake tarehe 07 Oktoba 2025.


Tukio hilo limevutia hisia za wananchi waliokuwa kandokando ya barabara, ambapo wengi walionesha furaha na kupongeza unyenyekevu wa viongozi hao, waliokuwa wakijumuika nao katika shughuli za kawaida za maisha ya kila siku.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI