NA MATUKIO DAIMA MEDIA
WASHITAKIWA 10 wakiwemo wanawake 6 wamefikishwa mbele ya hakimu mkazi wa wilaya ya Iringa Rehema Mayagilo wakituhumiwa kumuua kwa makusudi kijana Yohana Fredy Mgaya wakimtuhumu kuiba Parachichi.
TAZAMA FULL VIDEO WASHITAKIWA 10 WA MAUAJI WAKIFIKISHWA MAHAKAMANI BOFYA LINK HII
Wakili wa serikali Sauli Makoli ameiambia mahakama hiyo leo Alhamisi September 24 mwaka huu kuwa washitakiwa walitenda kosa hilo la mauaji Septemba 11 mwaka huu eneo la Don Bosco mjini Iringa.
Aliwataja washitakiwa hao wanaokabiliwa na kesi ya mauaji namba PI 23302/25 kuwa ni Farida Samweli Kamwagira, Rahabu Jacob Nisilu, Mussa Rashid Chondoma,
Vasco Disti Sanga maarufu kwa jina la Mkenya, Teodosia Silvesta Msilu, Bosco Juma Kabogo, Zawadi Patrick Msele,Velina Samson Chadewa na Erasto Sevelin Kilamililo huku washitakiwa wote wakikana shitaka dhidi yao.
Hata hivyo upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Akiahirisha kesi hiyo hakimu Rehema Mayagilo alisema kuwa kesi hiyo haina dhamana hivyo washitakiwa wataendelea kukaa mahabusu hadi Tarehe 8 Oktoba kesi hiyo itakapokuja kwa kutajwa tena.
0 Comments