Header Ads Widget

WANANCHI WATAKIWA KUWAPA USHIRIKIANO WAWEKEZAJI.

 

Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Ismail Alli Ussi (kushoto) akiwezindua kituo cha Mafuta cha Buha Energy katika kijiji cha Kasange Halmashauri ya wilaya Kigoma (kulia) Mkuu wa wilaya Kigoma Rashid Chuachua.



Na Fadhili Abdallah, Kigoma


KIONGOZI wa mbio za mwenge wa uhuru Ismail Alli Ussi amewataka wananchi kuwapa ushirikiano wawekezaji wanaotekeleza miradi katika maeneo yao kwani miradi hiyo imekuwa na msaada mkubwa katika kuisaidia serikali kusogeza hudumwa kwa wananchi.


Akizundua kituo cha mafuta cha Buha Energy kilichopo kijiji cha Kasange  Halmashauri ya wilaya Kigoma wakati mwenge wa uhuru ulipozindua kituo hicho ambaco ni kituo pekee katika barabara ya Kigoma kuelekea Manyovu wilaya ya Buhigwe mpakani mwa Tanzania na Burundi.


Kiongozi huyo alisema kuwa taarifa alizonazo ni kwamba hakuna kituo chochote cha mafuta katika barabara hiyo ya kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 65 hivyo magari yote ni lazima yajaze mafuta Kigoma Mjini au wilaya ya Buhigwe hivyo uwepo wa kituo hicho kumesogeza huduma karibu na wananchi.


Alisema kuwa serikali imeweka mazingira mazuri kwa wawekezaji na ndiyo wanawekeza kwenye maeneo mbalimbali hivyo wananchi nao hawana budi kushirikiana nao kwa kutoa au kuwauzia maeneo ya uwekezaji ili wafanye shughuli zao kwani ndani yake wananchi wananufaika kwa kupata ajira.


 

Akitoa taarifa kwa kiongozi  wa mwenge wa uhuru mwaka huu,  Meneja wa kituo cha mafuta cha Buha Energy, Justin Evarist alisema kuwa uwekezaji huo unafuatia fursa iliyopo na mazingirjia mazuri ya uwekezaji yanyojumuisha hali nzuri ya ulinzi na usalama inayoruhusu shughuli za uwekezaji na biashara kufanyika.


Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Kigoma,Rashid Chuachua alisema kuwa barabara hiyo ni muhimu kwa uchumi na ushirikiano baina ya Tanzania na Burundi hivyo kutekelezwa kwa mradi huo kunasogeza huduma karibu ambayo imekuwa na mahitaji makubwa kwa vyombo vya usafiri vinavyotumia njia hiyo.


Mwisho.


Mkurugenzi wa kituo cha mafuta cha Buha Energy, Justin Evarist (kulia) akitoa maelezo kwa Kiongozi wa mwenge wa uhuru wakati Mwenge ulipozindua kituo hicho mapema leo.


Kiongozi wa mwenge wa uhuru Ismail Alli Ussi (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha mafuta cha Buha Energy kilichopo kijiji cha Kasange Halmashauri ya wilaya Kigoma wakati mwenge wa uhuru ulipotembelea na kuzindua kituo hicho.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI