Header Ads Widget

BUTEMBO AZINDUA KAMPENI ZA UDIWANI MAGOMENI, AHAIDI KUWEKA TAA KWENYE MITAA YOTE




Na. Mwandishi Wetu, Kinondoni.

MGOMBEA Udiwani wa Kata ya Magomeni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Noordin Yusuph Hassan 'Butembo' amezindua rasmi kampeni zake huku akiomba kura za kishindo ili kuendelea alipoishia ikiwemo kuweka taa katika barabara zote za mitaa. 

Mhe. Butembo amesema hayo mapema leo Septemba 20, 2025 katika uzinduzi uliofanyika kwenye viwanja vya Mtaa wa Idrisa Magomeni mapipa.

Ambapo amesema ameingia Kata hiyo mwaka 2020-2025 na kutekeleza Ilani ya CCM kwa miradi mbalimbali kwa asilimia kubwa na sasa akiomba kwa awamu nyingine kumalizia asilimia  iliyobakia.


"Nimefanikiwa kuendeleza na kuanzisha masuala ya kimaendeleo tokea nilipoingia awamu ya kwanza.

Suala la Elimu kama shule na miundombinu yake, lakini pia huduma za Afya na miundombinu yake imeweza kufikiwa na kutekelezwa, Tunashukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini pia Rais wetu Mhe Samia Suluhu Hassan ambaye pia namuombea kura za kishindo pamoja na mgombea Ubunge Mhe Tarimba Abbas Tarimba.

Huduma za Kijamii tuliahidi kujenga ukuta kwenye makaburi ya Ndugumbi, lakini pia ngazi kwa makazi ya mabondeni na maeneo mengine.

Lakini pia mwaka huu kazi ya kwanza ambayo nilikuwa nimebakiza, mkinichagua tu, nitaanza na kuweka taa za barabarani kwenye mitaa yote." Amesema Butembo.




Awali mgeni rasmi katika uzinduzi huo wa Kampeni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Ndugu. Shaweji Mkumbura amewahakikishia Wana Magomeni kuwa CCM itaendelea kushirikiana na Wananchi wake katika maendeleo na amewataka kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29, kwa kupiga kura za NDIYO kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa CCM.

"Wana Magomeni mimi ni mwenzenu, nimetokea kea hapa na nimewahi kuwa Diwani, Butembo amenipokea kijiti na ameendeleza nilipoishia na sasa anakuja kwenu tena kuendeleza zaidi, tumpe kura za kutosha za ndiyo, lakini pia kero ya mafuriko sasa basi kwani Serikali inaleta mradi wa daraja la juu hapa Magomeni mpaka jangwani, hii ni sera ya CCM katika kufikia malengo kwa Wananchi wake." Amesema Ndugu Shaweji Mkumbura.

Kata ya Magomeni ina jumla ya mitaa mitano, ikiwemo Mtaa wa Sunna, Dossi, Makuti A, Mtaa wa Idrisa na Makuti B.













Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI