Na Matukio daima media
Wanachama na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameonesha matumaini makubwa kwa Mgombea wa Urais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, wakisema kuwa katika kipindi kifupi cha uongozi wake ameleta mageuzi makubwa katika sekta muhimu za kijamii na kiuchumi.
Wamesema hatua zilizochukuliwa na Dkt. Mwinyi katika kuboresha elimu, afya, barabara, bandari na viwanja vya ndege ni ushahidi tosha wa dira yake ya maendeleo na uthubutu wa kuijenga Zanzibar yenye ustawi kwa wananchi wote.
0 Comments