Mgombea udiwani kata ya isamilo Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Charles Nyamasiriri kupitia Chama Cha Mapinduzi.Na chausiku said
Matukio Daima Mwanza.
Mgombea udiwani kata ya Isamilo Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Charles Nyamasiriri, ameahidi kushirikiana na wananchi wa kata hiyo kuendeleza miradi ya maendeleo na kutatua changamoto zilizobakia.
Akizungumza jana Septemba 14 katika viwanja vya shule ya msingi Kileleni, wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za udiwani, alieleza utekelezaji wa miradi iliyofanyika katika kata hiyo katika kipindi cha uongozi wake.
Mwenyekiti Wilaya ya Nyamagana chama Cha mapinduzi (CCM) wa pili kutoka kushoto Peter Bega akimnadi mgombea Udiwani kata ya lsamilo Charles Nyamasiriri
Nyamasiriri alieleza kuwa awali kulikuwa na changamoto nyingi katika kata hiyo ikiwemo ukosefu wa ofisi ya mwenyekiti wa mtaa wa Isamilo, lakini kwa sasa ofisi mpya imejengwa iliyogharimu kiasi Cha Sh Milioni 30, pia Halmashauri ilitenga kiasi Cha Sh Milioni 340 kwa ajili ya mikopo ya wanawake, vijana na makundi maalumu ambapo vikundi zaidi ya 44 vilinufaika.
Baadhi ya wananchi wa kata ya isamilo walioudhulia katika ufunguzi wa kampeni za uchaguzi wa udiwani uliofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi kileleni
Kuhusu sekta ya afya, Nyamasiriri alisema kata hiyo sasa ina zahanati inayotoa huduma bora, huku katika elimu ya sekondari vyumba vya madarasa zaidi ya 14 vimejengwa na kuondoa changamoto iliyokuwepo. Hata hivyo, alibainisha kuwepo kwa changamoto katika shule ya msingi Kileleni na kueleza kuwa tayari serikali kuu imeombwa Sh milioni 470 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya msingi.
Katika sekta ya maji, alisema bado changamoto ipo lakini wananchi wanapata huduma kwa bei nafuu Kwa kuunganishiwa maji kiasi cha Sh 21,000, huku akihaidi kuwa endapo akipewa tena ridhaa ya kuongoza, atahakikisha tatizo la maji linamalizika kupitia chanzo kipya cha maji cha Butimba kwa kushirikiana na mbunge mtiania wa Jimbo la Nyamagana.
Aidha, Nyamasiriri alisema hapo nyuma maeneo ya milimani yalikuwa hayajapimwa lakini sasa yamepimwa na leseni za makazi zimetolewa kwa wananchi. Kuhusu miundombinu ya barabara, alieleza kuwa fedha za maendeleo zilizotolewa ni Sh Bilioni 3.271 ambazo zimeelekezwa kwenye miradi mbalimbali.
Mgombea Ubunge Jimbo la Nyamagana kupitia chama Cha mapinduzi (CCM) John Nzilanyingi akizungumza na wananchi wa kata ya lsamilo na kuomba ridhaa ya kumchagua ili aweze kuipeperusha bendera ya chama hicho
Amefafanua barabara zilizojengwa kuwa ni pamoja na ya Genge la Washashi kwa kiwango cha zege na mawe, barabara ya International kuelekea Pepsi kwa kiwango cha lami, Kondeko iliyojengwa kwa kuchangia wananchi na msaada wa mbunge aliyemaliza muda wake, barabara ya Kivumbini na ya Genge la Emma kwa kiwango cha mawe na zege.
Kwa upande wake, mgombea mbunge Jimbo la Nyamagana, John Nzilanyingi, alisema vipaumbele walivyonavyo ni kuimarisha miundombinu ya barabara, maji na elimu, akisisitiza kuwa kata ya Isamilo itakuwa ya kwanza kunufaika na miradi hiyo.
Nzilanyingi alibainisha kuwa serikali ya awamu ya sita kupitia ilani ya CCM ya uchaguzi wa mwaka 2025–2030 imeweka mkakati wa kuhakikisha wananchi wote wanapata maji safi na salama pamoja na kuboresha elimu ya msingi kwa kujenga madarasa, kuongeza madawati na kujenga shule mpya.
Aidha, aliahidi kushirikiana na diwani mtarajiwa ili kuhakikisha Jiji la Mwanza linatenga fedha za mikopo ya asilimia 10 kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ili vikundi vyote vilivyosajiliwa viweze kunufaika.
0 Comments