Header Ads Widget

WAJASILIAMALI WANAOZINGATIA UBORA WAONGEZEKA

 

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Shirika la viwango nchini (TBS) limesema kuwa kumekuwa na idadi kubwa ya watanzania wajasiliamali ambaao wanatumia alama ya ubora ya taasisi hizo kwa ajili ya bidhaa zao jambo linalochangia ongezeko kubwa la bidhaa za tanzaniaa zinazovuka mpaka kuwa na viwango vunavyokubalika.

Afisa Udhibiti ubora wa TBS Kanda ya Magharibi, Peter Musiba alieleza hayo wakati wa mafunzo kwa wajasiliamali wa mkoa Kigoma walioshiriki kwenye mbio za mwenge wa uhuru Manispaa ya Kigoma Ujiji ambao walikuwa na mabanda yaliyokuwa yakiuza bidhaa mbalimbali kwenye mkesha wa mwenge kwwenye manispaa hiyo.

Musiba alisema kuwa mkoa Kigoma ni moja ya mikoa ambayo inapakana na nchi nyingi hivyo wajasiliamali wana ulazima mkubwa wa kuzingatia ubora wa bidhaa zao ili kuwasaidia kupata masoko ya uhakika kwa bidhaa.

Mmoja wa wajasiliamali walioongea na waandishi wa habari wakati wa mafunzo yaliyotolewa na TBS,  Angelina Lebel alisema kuwa amekuwa akufanya biashara kwa nchi za ukanda wa maziwa makuu na Kenya kwa sasa hajapata nembo ya ubora lakini mafunzo ya TBS yamemjenga na yupo mbioni kupata nembo ya ubora baada ya kuanza mchakato akiamini itafanya bidhaa zake kuaminika katika soko la nje.

Akizungumza katika mbio za Mwenge katika manispaa ya Kigoma Ujiji Kiongozi wa mwenge wa uhuru Ismail Alli Ussi alisema kuwa serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wajasiliamali ili waweze kufanya shughuli zao kwa tija kubwa, kutoa mikopo sambamba na kuwaunganisha na masoko ya ndani na nje ili shughuli za ujasiliamali ziwe na mchango mkubwa kwa Taifa.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI