Rais wa Marekani Donald Trump amelaani kifo cha Charlie Kirk Kirk aliyekuwa alikuwa mmoja wa wanaharakati wahafidhina (Conservative) mashuhuri na mwanahabari nchini Marekani na mshirika wa kutumainiwa wa Rais Donald Trump.
Ameyataja mauaji ya Charlie Kirk 'wakati wa giza kwa Marekani' huku msako mkali ukiendelea kuwapata wahusika wa shambulio hilo, lililowashutua Wamarekani.
Charlie Kirk , 31, aliuawa kwa kupigwa risasi alipokuwa akizungumza katika hafla katika Chuo Kikuu cha Utah Valley.
Kirk alipigwa risasi moja shingoni, video iliyothibitishwa na kitengo cha uhakiki wa habari cha BBC -BBC Verify, imeonyesha.Hakuna mtu mwingine aliyepigwa risasi wakati wa tukio hilo. Mshambuliaji bado hajakamatwa.
Mke na watoto wa Kirk walikuwepo wakati wa ufyatuaji risasi, kulingana na Seneta wa Oklahoma Markwayne Mullins.Bado hakuna sababu inayojulikana ya upigaji risasi huo
Mnamo 2012, akiwa na umri wa miaka 18, alianzisha shirika la Turning Point USA, shirika la wanafunzi ambalo linalenga kueneza maadili ya kihafidhina katika vyuo vya Marekani.
Mitandao yake ya kijamii na podikasti ya kila siku iliyojulikana mara nyingi alikuwa akijadiliana na wanafunzi kuhusu masuala kama vile utambulisho wa watu waliobadili jinsia, mabadiliko ya hali ya hewa, imani na maadili ya familia.
Kirk alikuwa ameoa na alikuwa na watoto wawili wadogo, ambao walikuwa naye wakati wa tukio la ufyatuaji risasi.
Mauji yake pia yamelaaniwa na viongozi mbali mbali wa kisiasa wa Marekani na nje ya nchi, walioyataji kama yasiyokubalika na kutoa wito wahusika waadhibiwe ili kuyakomesha.
0 Comments