Header Ads Widget

QATAR YASEMA 'TUMESALITIWA'

 

Qatar ilitoa taarifa yenye maneno makali mapema Alhamisi asubuhi ikilaani matamshi ya Netanyahu kuhusu uwepo wa ofisi ya Hamas, na kuyaita "ya kutojali."

Waziri Mkuu wa Qatar Mohammed bin Abdulrahman Al Thani alisema: "Siwezi kupata maneno ya kuelezea kiwango cha hasira zetu. Huu ni ugaidi wa serikali. Tumesalitiwa."

Qatar imesema kuwa "Netanyahu anajaribu kuharibu kila fursa kwa utulivu na amani," baada ya kufanya "shambulio la wazi" dhidi ya viongozi wa Hamas huko Doha.

Qatar iliongeza kuwa ni "ufahamu wa umma" kwamba maafisa wa Qatar wanakutana na viongozi wa Hamas, kama sehemu ya jukumu la Qatar kama mpatanishi katika mzozo unaoendelea wa Mashariki ya Kati.

Doha ilifafanua kuwa "kila kitu kuhusu mkutano huu kinajulikana kwa Waisraeli na Wamarekani, si jambo tunaloweza kuficha... Hakuna sababu ya kuuchukulia kuwa unahifadhi ugaidi.''

Haya yanajiri huku mamlaka ya Qatar ikisema bado inawasaka watu wawili waliotoweka na kuyatambua mabaki ya miili ya binadamu baada ya shambulio la Israel kuwalenga viongozi wakuu wa Hamas mjini Doha siku ya Jumanne.

Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kuwa kuna wasiwasi katika duru za kijeshi za Israel kwamba shambulio hilo lenye utata mkubwa halikufanikiwa.

Wizara ya mambo ya ndani ya Qatar imeitambua miili ya wanachama watatu kati ya watano wa ngazi ya chini wa Hamas ambao kundi lenye silaha la Palestina lilisema waliuawa pamoja na afisa wa usalama wa Qatar.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI