Header Ads Widget

PUTIN APINGA MPANGO WA USALAMA WA MATAIFA YA MAGHARIBI NCHINI UKRAINE

 

Rais wa Urusi Vladimir Putin amepinga pendekezo ya nchi za Magharibi la "kupeleka jeshi" nchini Ukraine siku moja baada ya kusitishwa kwa mapigano, kufuatia mkutano wa kilele wa Paris unaolenga kukamilisha mipango ya dhamana ya usalama.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema washirika 26 wa Ukraine wamejitolea rasmi kupeleka wanajeshi "kwa nchi kavu, baharini au angani" kusaidia kudumisha usalama mara baada ya mapigano kusitishwa. Hakueleza kwa undani nchi yoyote iliyohusika.

Putin alitaka kukomeshwa kwa mpango huo, akionya kwamba wanajeshi wowote watakaopelekwa nchini Ukraine watakuwa "lengo halali", haswa ikiwa watajitokeza muda huu, ingawa mpango wa kuwapeleka kwa sasa hujafikiwa.

Matumaini ya kusitishwa kwa mapigano kwa sasa yamefifia, baada ya mkutano wa kilele wa mwezi uliopita huko Alaska kati ya Putin na Rais wa Marekani Donald Trump kuibua kwa ufupi matumaini ya kiongozi huyo wa Urusi kukutana na mwenzake wa Ukraine na Volodymyr Zelensky na uwezekano wa makubaliano ya amani kufikiwa.

Putin alisema siku ya Ijumaa yuko tayari kwa mawasiliano na kiongozi huyo wa Ukraine "lakini sioni sababu ya kufanya hivyo kwa nini? Kwa sababu ni vigumu kufikia makubaliano na Ukraine kuhusu masuala muhimu".

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI