Magwiji wa ndondi Mike Tyson na Floyd Mayweather kukutana ulingoni mwaka 2026, kulingana na kampuni ya ndondi ya CSI Sports.
CSI Sports tayari imetangaza pambano kati ya Tyson, ambaye atatimiza umri wa miaka 60 mwaka ujao, na Mayweather, 48, lakini haikutoa mahali au maelezo yoyote ya tarehe, zaidi ya kusema kwamba pigano hilo lifanyika mwaka ujao.
Bingwa wa zamani wa uzani wa juu duniani Tyson, ambaye alipoteza pointi kwa Jake Paul katika pambano la raundi nane mnamo Novemba 2024, alisema: "Pambano hili si jambo ambalo ulimwengu wala sikuwahi kufikiria lingetokea au lingeweza kutokea.
"Ndondi imeingia katika enzi mpya ya kutotabirika - na pambano hili halitabiriki kabisi.
"Bado siamini kwamba Floyd anataka kufanya hivi. Itakuwa hatari kwa afya yake, lakini anataka kufanya hivyo, kwa hivyo imesainiwa na itafanyika."
Mayweather alishinda mataji ya dunia katika aina tano ya viwango vya uzito tofauti bila kushindwa katika maisha yake ya mapambano 50 ambayo yalimalizika kwa ushindi dhidi ya nyota wa MMA Conor McGregor mnamo 2017.
0 Comments