Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro (wa kulia) akitoa taarifa ya miradi itakayopitiwa na mwenge wakati akipokea mwenge wa uhuru kutoka mkoani Kagera mapema leo asubuhi
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Mwenge wa uhuru umeanza mbio zake mkoani Kigoma jana ambapo utapita kwenye miradi 56 yenye thamani ya shilingi Bilioni 64.7 ambapo ukiwa mkoani humo mwenge huo wa uhuru utatembea kilimotea 777.1 katika halmashauri nane za mkoa Kigoma.
Mkuu wa mkoa Kigoma,Balozi Simon Sirro alisema hayo akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa Mkuu wa mkoa Kagera,Fatuma Mwassa katika makabidhiano yaliyofanyika katika kijiji cha Nyakibuye wilaya Kakonko mkoani Kigoma.
Mkuu wa mkoa Kagera Fatma Mwassa (kushoto) akikabidhi mwenge wa uhuru kwa Mkuu wa mkoa Kigoma Balo, Simon Sirro katika makabidhiano yaliyofanyika kijiji cha Nyabibuye wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Leo asubuhi
Balozi Sirrtio alisema kuwa katika miradi itakayopitiwa na mwenge Miradi 16 itawekewa mawe ya msingi,a mmojutafunguliwa, 27 kuzinduliwa na 12 itatembelewa.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa katika miradi inayotembelea na mwenge Wananchi wamechangia kiasi cha shilingi milioni 283, halmashauri shilingi bilioni 1.6, wahisani shiliingi Bilioni 53.1 na serikali kuu ni bilioni 6.6.
Mwenge wa uhuru ukianza mbio za siku nane mkoani Kigoma
Katika siku ya kwanza ya mbio zake mkoani Kigoka Mwenge wa uhuru ulikimbizwa katika wilaya ya Kakonko ambapo Mkuu wa wilaya hiyo Evance Malasa alisema kuwa ukiwa wilayani humo mwenge huo wa uhuru utatembelea miradi saba yenye thamani ya shilingi bilioni 2.2 ukikimbizwa kwa umbali wa kilometa 135.
0 Comments