Na COSTANTINE MATHIAS, Itilima-Simiyu.
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Itilima (CCM), Njalu Daud Silanga ameendelea na kampeni ya kuzitafuta kura za ushindi wa Chama Cha Mapinduzi kata kwa kata ili kuhakikisha Mgombea Urais Samia Suluhu Hassan, Ubunge (Njalu) na Madiwani wa CCM wanapata kura za kutosha.
Aidha, amewataka wananchi, wapenzi na wakereketwa wa CCM kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi kwa kuhakikisha wanajitokeza kupiga kura Oktoba 29, 2025 ili chama Tawala kuendelee kuwahudumia na kuwaletea Maendeleo.
Njalu amesema hayo jana kwa nyakati tofauti wakati akinadi sera za CCM kwa wakazi wa kata ya Mwamtani, Bumera, Ikindilo na Budalabujiga wilayani Itilima Mkoani Simiyu.
"Mimi bado kijana, sitaki kuwa mbunge Muongo ambaye badae mtaninyoshea kidole kwa sababu sijatekeleza, Kila ninachokisema basi mjue kweli kitafanyika...ombi langu tujitokeze tarehe 29, Oktoba tukampe kura nyingi Dkt. Samia Suluhu Hassan Mgombea Urais,Tupige kura ya ndiyo kwa Mbunge na tuwape kura za kutosha madiwani wa CCM" amesema Njalu.
Mwisho.
0 Comments