Na,Jusline Marco:Arusha
Maafisa na Askari wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Karatu, wadau wa Uhifadhi na Utalii pamoja na Wananchi wameungana kuadhimisha siku ya Faru Duniani kwa kufanya Mbio za kilomita 5 katika mji wa Karatu zenye lengo la kuhamasisha shughuli za uhifadhi wa Mnyama Faru.
Katika kuadhimisha Siku hiyo NCAA imefanya shughuli mbalimbali ikiwepo utoaji wa elimu ya uhifadhi wa Faru kwa jamii, kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira, maonesho ya uhifadhi wa Faru pamoja na Michezo mbalimbali yenye lengo la kuhamasisha uhifadhi wa Faru.
Kauli Mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Faru ni "Tuhakikishe aina tano za Faru waliopo duniani wanaishi"
0 Comments