Header Ads Widget

RIDHIWANI KIKWETE KUSIMAMIA UJENZI WA SHULE MPYA ZA SEKONDARI 14 CHALINZE.

 

Na Mwandishi Wetu, Matukio Daima Media.

Chalinze.MGOMBEA Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwani Kikwete amesema atahakikisha anasimamia ujenzi wa Shule mpya 14 za Sekondari ili watoto wapate fursa za elimu.

Kikwete amesema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni za Udiwani Kata ya Kiwangwa na kumnadi mgombea Udiwani wa CCM Kata hiyo Malota Kwaga.

Alisema kuwa elimu ni mkombozi kwa kizazi kijacho hivyo hicho ni kipaumbele kwa lengo la kuleta mabadiliko na wananchi kuweza kujiletea maendeleo.

"Kwa Kiwangwa yatajengwa madarasa 24 na hii inafanywa kwa kuwa elimu ndiyo msingi wa kila jambo kwa kuwa na shule nzuri hivyo elimu ni kipaumbele kikubwa",alisema Kikwete.

Aidha alisema kuwa ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari iliyopewa jina lake iliyokamilika hivi karibuni na sasa inatumika ni kielelezo cha uwekezaji kwenye sekta ya elimu.

"Tunaishukuru serikali kwa ujenzi huo kwani umeipunguzia mzigo shule ya sekondari ya Kiwangwa ambayo ilikuwa imezidiwa na wanafunzi hivyo wananchi wanapaswa kumpa kura za kishindo Mgombea wetu wa Urais Dk Samia Suluhu Hassan na mimi na diwani wetu ili tuendeleze mafanikio haya,"alisema Kikwete.

Kwa upande wake Mgombea Udiwani Kata ya Kiwangwa Malota Kwaga alisema kuwa ujenzi wa bwalo kwenye shule ya sekondari ya Kiwangwa, ujenzi wa maktaba, ujenzi wa maktaba shule za Kiwangwa na Ridhiwani Kikwete Sekondari, ujenzi matundu ya vyoo 26, ujenzi wa nyumba 25 za walimu na ujenzi wa barabara na taa za barabarani.

Kwaga alisema kuwa pia akifanikiwa kuchaguliwa atasimamia moja ya vitu atakavyosimamia ni ukamilishwaji wa kituo cha afya ambapo serikali imetoa shilingi milioni 700 na kikikamilika kitapatiwa gari la wagonjwa na watabebwa bure.

 mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI