DNA kwenye taulo iliyozungushiwa bunduki inayoshukiwa kutumika kumuua Charlie Kirk imelingana na DNA ya mshukiwa aliye kizuizini, mkurugenzi wa FBI amesema siku ya Jumatatu.
Tyler Robinson, 22, alikamatwa kufuatia kifo cha Kirk katika hafla kwenye Chuo Kikuu cha Utah Valley mnamo Jumatano. Bunduki aina ya ‘bolt-action’ ilipatikana karibu na eneo la tukio huku bisibisi ikionekana kwenye paa ambapo risasi iliyomuua mfuasi huyo ilifyatuliwa.
"Naweza kusema leo kwamba DNA iliyokuwa kwenye taulo iliyofungwa kwenye bunduki na DNA kwenye bisibisi zimelingana na ile ya mshukiwa aliye kizuizini," Kash Patel aliiambia Fox and Friends.
Mashtaka rasmi yanatarajiwa wiki hii.
Mkurugenzi wa FBI - ambaye anatarajiwa kuhojiwa katika kikao cha Bunge siku ya Jumanne - pia alitaja barua iliyogunduliwa nyumbani kwa mshukiwa, ambayo iliapa "kumuondoa" Kirk.
"Kimsingi inasema... 'Nina fursa ya kumuondoa Charlie Kirk', na nitatumia fursa hiyo. Maelezo hayo yaliandikwa kabla ya Kirk kupigwa risasi," alisema Patel.
Aliongeza, "ingawa imeharibiwa, tumepata ushahidi wa kitaalamu wa barua hiyo".
0 Comments