Header Ads Widget

MAZOEZI YA KIJESHI YA BELARUS NA URUSI YAONEKANA KUTOA UJUMBE KWA ULAYA

Vikosi vya kijeshi vya Belarusi na Urusi vinashiriki katika mazoezi ya pamoja kwenye uwanja wa Borisovsky, tukio ambalo linashuhudiwa na vyombo habari vya kimataifa.

Katika uwanja mkubwa wa maili 45 (72km) kutoka mji mkuu wa Belarus Minsk, vita vinaendelea.

Kuna milipuko mikubwa huku washambuliaji wa Sukhoi-34 wakidondosha mabomu. Moshi mwingi unafanya anga kuwa giza.

Eneo lote linatoa mwangwi na makombora ya mizinga yanayolipuka. Helikopta ya kijeshi ya kivita inajiunga na shambulio hilo, huku ndege zisizo na rubani zikitanda angani kutazama uharibifu.

Haya yote ni mazoezi tu. Ni sehemu ya mazoezi ya kijeshi ya Zapad-2025 ("West 2025"). Maafisa wengine wa kijeshi kutoka balozi mbalimbali pia walikuwepo kushuhudia kinachoendelea.

Haya ni mazoezi yaliyopangwa ya "West 2025" ambayo hufanyika kila baada ya miaka minne.

Moscow na Minsk zinashikilia kuwa mazoezi hayo ni ya kujilinda tu, kwamba yameandaliwa ili kuimarisha usalama wa Urusi na Belarusi na kukabiliana na tishio lolote la nje linaloweza kutokea.

Madai kama hayo yalisikika miaka mitatu na nusu iliyopita.

Mnamo Februari 2022 BBC ilitembelea Belarusi ili kuripoti juu ya mazoezi ya kijeshi ya Belarusi-Urusi.

Zoezi hilo lilipokamilika, badala ya kurejea nyumbani wanajeshi wa Urusi walivamia nchi jirani ya Ukraine kutoka eneo la Belarus.

Wakati huu Belarus inasisitiza kuwa haina chochote cha kujificha.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI