Erica Kirk, mke wa mwanaharakati Charlie Kirk, ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi, aliwaambia hadhira katika sherehe iliyohudhuriwa na makumi ya maelfu ya watu, akiwemo rais Donald Trump wa Marekani a watu wengine maarufu kama vile Elon Musk, kwamba aliongozwa na mafundisho ya Kikristo kumsamehe mtu huyo aliyemshambulia na kumuua mumewe.
Erica Kirk, ambaye ana shahada ya chuo kikuu ya theolojia na huendesha podcast inayohusu mafundisho ya Kikristo, alisema Jumapili, Septemba 21, baada ya kusoma vifungu kutoka katika Biblia, kwamba kama mumewe, Charlie Kirk, angekuwa hai, angekubaliana naye juu ya "kuwapenda maadui zetu na kuwapenda wale wanaotutesa."
Baada ya ibada ya kidini ambayo ilikuwa sehemu kubwa ya sherehe ya kumkumbuka Charlie Kirk huko Arizona, Marekani na mwishoni mwa hotuba ya Erica Kirk, Donald Trump alipanda jukwaani na kuiambia hadhira, "Charlie bila shaka angejifunza fahari kubwa kuwasikia watu wakimpa Mungu utukufu leo."
Aliongeza: "Tunahitaji kuirejesha dini nchini Marekani, na tunataka kumrejesha Mungu katika ardhi yetu nzuri kama ilivyokuwa hapo awali."
Mhariri wa BBC wa Amerika Kaskazini, Sarah Smith, ambaye alihudhuria hafla hiyo, alisema misa hiyo ilikuwa zaidi kama mkutano wa kisiasa kuliko misa ya kumbukumbu ya msiba.
Mbali na Donald Trump, makamu wa rais wa Marekani, J.D. Vance, na viongozi wengine wakubwa Marekani walihudhuria tukio hilo.
0 Comments