Leo jioni, tarehe 22 Septemba 2025, hafla ya utoaji wa tuzo ya Ballon d’Or itafanyika huko ThĂ©Ă¢tre du ChĂ¢telet jijini Paris, ambapo washindi wa tuzo za wanasoka bora wanaume na wanawake kwa msimu wa 2024–25 watatangazwa.
Tuzo hizi zinachukuliwa kama heshima kubwa zaidi katika soka duniani, na mashabiki na vyombo vya habari vinasubiria kwa hamu matokeo.
Kwa upande wa wanaume, Ousmane DembĂ©lĂ© wa Paris Saint-Germain (PSG) anatajwa kupewa nafasi kubwa. Msimu wake wa 2024–25 ulifunga mabao 21 katika ligi kuu ya ufaransa (Ligue 1), akisaidia mabao 14, na mchango mkubwa katika kutwaa mataji ya ligi kuu, Ligi ya Mabingwa ya Ulaya, na kombe la klabu za dunia.
Kylian MbappĂ© wa Real Madrid pia yupo kwenye kinyang’anyiro, baada ya kuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Hispani (La Liga) kwa kufunga mabao 50 kwa timu yake ya taifa ya Ufaransa.
Mohamed Salah wa Liverpool ni mchezaji mwingine anayepewa nafasi kubwa, akisaidia Liverpool kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza (EPL) na kushinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu wa ligi hiyo kwa mara ya pili. Raphinha na Lamine Yamal wa Barcelona pia wanashindania, wakiwa na mchango mkubwa katika kushinda mataji ya La Liga, Copa del Rey na Supercopa de España. Harry Kane wa Bayern Munich ni miongoni mwa wachezaji waliothibitisha ubora wao, akiongoza timu yake kutwaa ubingwa wa Bundesliga.
Kwa upande wa wanawake, Aitana BonmatĂ wa Barcelona anapewa nafasi kubwa kushinda tuzo ya Ballon d’Or FĂ©minin.
Hafla ya utoaji wa tuzo itaanza saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki
0 Comments