Header Ads Widget

PROF. MKUMBO AZINDUA KAMPENI ZA UDIWANI UBUNGO, AMWOMBEA KURA RAIS SAMIA

Mgombea wa Ubunge Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya CCM, Professa Kitila Mkumbo (kushoto ) akimnadi mgombea Udiwani wa Kata ya Ubungo, Ndugu Jaffary Nyaigesha katika uzinduzi wa kampeni za Kata hiyo jana Septemba 21,2025 katika viwanja vya Ubungo maji.


Na. Mwandishi Wetu, Ubungo.

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Ubungo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Professa Kitila Alexander Mkumbo amemnadi mgombea Udiwani wa Kata ya Ubungo, Ndugu Jaffary Nyaigesha katika uzinduzi wa kampeni za Kata hiyo jana Septemba 21,2025 katika viwanja vya Ubungo maji.

Mhe Prof. Kitila Mkumbo ambaye pia anagombea Jimbo la Ubungo, amepata wasaha wa kumuombea kura Diwani Nyaigesha pamoja na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kupata kura nyingi hiyo Oktoba 29 mwaka huu.

"Namuombea kura za kishindo za Ndiyo Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini pia kura za Ndiyo kwa mgombea Udiwani Nyaigesha na kura za Ndiyo kwa mimi Mbunge wenu Kitila Mkumbo." Amesema Prof. Kitila Mkumbo.





Aidha, amewahakikishia Wana Ubungo kuwa suala la mradi wa Mwendokasi limepatiwa ufumbuzi na mwekezaji binafsi amepatikana

"Nafahamu hapa mradi wa mabasi ya Mwendokasi unaleta shida ila kwa sasa shida hiyo inaenda kuisha,

Jumla ya mabasi 177 yataletwa nchini mwanzoni mwa Novemba mwaka huu, utasaidia usafirishaji kuanzia Kimara hadi katikati ya mji ikiwemo Kariakoo, Kivukoni.

Mabasi haya hayataendeshwa na Serikali, bali Sekta binafsi ilikuboresha huduma bora zaidi." Amesema Prof. Kitila Mkumbo.

Aidha, amewaambia Wananchi kuwa, Maendeleo ni mchakato endelevu. Hivyo wanaendelea kuomba kura na Serikali haisimami.

"tunaendelea kuomba kura na mengine yanaendelea. Kwa uwezo wa Mungu na uwezo wa kura za Watanzania Serikali itaendelea.

Mgombea Udiwani wa Kata ya Ubungo, Mhe Nyaigesha akinadi sera kwa Wananchi 

Mwenza wa Mgombea Udiwani wa Kata ya Ubungo, Mhe Nyaigesha akimuombea kura Rais, Mbunge na Diwani

Baadhi ya Madiwani wa viti maalum Jimbo la Ubungo wakiomba kura za Rais, Mbunge na Madiwani 

Prof. Mkumbo akimnadi mgombea Udiwani Nyaigesha 


"Tulikuwepo, tupo na tutakuwepo. Hatuwachi kushughulikia kero za Wananchi kwa sababu ya uchaguzi. Nchi zote zinapambana kupambanania Wananchi wake." Amesema Prof. Kitila Mkumbo.

Kwa upande wake, Mgombea Udiwani wa Kata hiyo, Mhe Nyaigesha amewaomba kura nyingi za Ndiyo Wananchi wa Ubungo ili aendelee kuwatumikia ikiwemo kuendeleza miradi iliyobakia na mipya.

Katika mkutano huo, amesema miradi mbalimbali imefanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya CCM ikiwemo shule, huduma za Afya na miundombinu katika mitaa yote ya Kata hiyo.










Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI