Wakazi wa Manispaa ya Morogoro wameingia katika majonzi kufuatia kifo cha mfanyabiashara mashuhuri na Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA), Bw. Mohamed Hood, (pichani) aliyefariki dunia Februari 2, 2026.
Mzee Hood (90) alijulikana sana katika sekta ya usafirishaji wa abiria, ambapo kwa miaka mingi alimiliki kampuni ya mabasi iliyokuwa ikihudumia safari za Dar es Salaam–Morogoro, Morogoro–Moshi–Arusha na mikoa mingine.
Kwa hiari yake mwenyewe, baadaye aliamua kusitisha biashara hiyo baada ya kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta hiyo nchini.
Mbali na shughuli za kibiashara, marehemu alikuwa pia mwanasiasa mkongwe, aliyewahi kuwa Diwani wa Kata ya Mji Mkuu, Manispaa ya Morogoro, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Wananchi, ndugu na marafiki wameendelea kumuenzi kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya jamii.
Mazishi ya marehemu yanatarajiwa kufanyika leo mjini Morogoro baada ya swala ya Adhuhuri.
Aidha, Mzee Hood amefariki dunia alasiri ya jumatatu ya February 02 na anategemewa kuzikwa leo jumanne ya Februari 03 katika makaburi ya kolla mjini Morogoro.
Taarifa za kudhoofika kwa afya ya mzee Hood zilipatikana takriban miaka miwili ya nyuma.
Hood alitamba katika nyanja ya usafirishaji nchini na hata nje ya mipaka ya nchi toka mwanzoni mwa miaka ya 90.
Poleni wanafamilia said Hood, Fesal Hood,Tiff Hood, Hood Hood na wakazi wa Morogoro .






0 Comments