Header Ads Widget

MAAFISA MIFUGO WAGAWIWA VISHIKWAMBI MBEYA DC.

 

  

Na Josea Sinkala, Mbeya

Maafisa Mifugo wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya mkoani Mbeya wamegawiwa vishikwambi kutoka Serikalini kwa ajili ya kuboresha huduma na utendaji kazi kwao katika kusimamia ipasavyo sekta ya kilimo kwa ujumla.

Halmashauri hiyo imewataka maafisa hao wa Mifugo kufanya kazi kwa ubunifu, weledi na uzalendo katika kuwahudumia wakulima ili kuchochea maendeleo kwenye sekta ya kilimo wilayani Mbeya.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Erica Yegella, ndiye amesema hayo wakati wa hafla ya ugawaji wa vishikwambi kwa maafisa Mifugo, vilivyotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ikiwa ni awamu ya pili ya kuwawezesha watendaji hao katika kazi zao za kusaidia wakulima. 


Pamoja na hayo, mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbeya Erica Yegella amesisitiza kuwa ofisi yake iko wazi kwa mtumishi yeyote mwenye wazo kwa Halmashauri katika kuiongezea mapato Halmashauri ya Mbeya huku pia akihimiza suala la ubunifu katika kupanga na kutekeleza shughuli za maendeleo. 

Bi. Erica amewataka maafisa hao kufanya kazi kwa ushirikiano baina yao na viongozi wengine kwenye maeneo yao ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma hasa katika Halmashauri hiyo ambayo ni wazalishaji wakubwa wa mazao mbalimbali.

Akizungumza kwa niaba ya maafisa Mifugo wa Halmashauri ya Mbeya, Afisa mifugo wa Halmashauri hiyo Gidion Mapunda amemshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbeya na Serikali kuu kupitia wizara ya kilimo kwa utoaji vifaa hivyo.

Mapunda ameahidi kuendeleza ushirikiano miongoni mwa wataalam hao na wananchi wanaowahudumia kwa kuhakikisha pia wanatumia vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kufikia maendeleo endelevu kwenye sekta ya kilimo.


Halmashauri ya wilaya ya Mbeya kwa sehemu kubwa inategemewa kwenye shughuli za kilimo na biashara hivyo maafisa kilimo wa Halmashauri hiyo kupewa vishikwambi kwa sehemu kubwa itawasaidia kuinua sekta hiyo kulima kisasa zaidi ikiwemo kutafuta mbinu mpya na bora katika kuboresha kilimo ikiwemo kutafuta dawa kwa ajili ya kuendeleza mazao mbalimbali ya chakula na biashara Mbeya vijijini.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI