Header Ads Widget

DKT. NCHIMBI AMNADI DKT DAVID MATHAYO MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SAME MAGHARIB


Na Ashrack Miraji Matukio Daima 

MGOMBEA Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John  Nchimbi, amewasili Wilaya ya Same kuwahutubia Wananchi wa jimbo la Same Magharibi kwenye mkutano wake mdogo,leo Jumapili Septemba 14,2025 mkoani Kilimanjaro.

Dkt.Nchimbi ambae ni mgombea mwenza wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan anaendelea na Mikutano yake ya kampeni mkoani Kilimanjaro,sambamba na kuwanadi Wagombea Ubunge wa Mkoa huo akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Same Magharibi,Ndugu Dkt.Mathayo David Mathayo pamoja na Madiwani.

Dkt. Nchimbi ameendelea kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2025-2030, ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa maendeleo katika miaka mitano ijayo.

Ngombea mwenza huyo amekuwa akitumia  nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani wa chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.





 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI